SALA KWA WATOTO NA VIJANA (#11216)

Ee Mungu!  Mlee mtoto huyu mchanga katika moyo wa upendo Wako, na umpe maziwa kutoka katika kifua cha Majaliwa Yako.  Palilia mche huu mchanga katika bustani ya waridi ya upendo Wako na umsaidie kukua kupitia manyunyu ya baraka Yako.  Mfanye mtoto wa Ufalme na umuongoze kwenye milki Yako ya mbinguni.  Wewe U mwenye nguvu na mwema, na Wewe U Mpaji, Karimu, Bwana wa Baraka zisizo kifani.

-`Abdu'l-Bahá
-----------------------

SALA KWA WATOTO NA VIJANA (#11217)

Ee Mungu! Wafundishe watoto hawa.  Watoto hawa ni miche ya kiunga Chako cha miti ya matunda, maua ya shamba Lako, waridi ya bustani Yako.  Acha mvua Yako iwanyeshee; acha Jua la ukweli liwaangazie na upendo Wako.  Acha upendo Wako uwaburudishe ili kwamba waweze kufundishwa, kukua na kuendelea na kuonekana katika uzuri wa juu kabisa.  Wewe u Mpaji!  Wewe u Mwenye huruma.

-`Abdu'l-Bahá
-----------------------

SALA KWA WATOTO NA VIJANA (#11218)

Ee Bwana!  Mfanye kijana huyu mwangavu na ujalie Baraka Yako juu ya kiumbe huyu mnyonge.  Umpe hekima, umjalie nguvu zaidi kwenye kila mapambazuko na umkinge katika kivuli cha ulinzi Wako ili aweze kuondolewa katika makosa, aweze kujiweka katika huduma ya Hoja Yako, aweze kuwaongoza wapotovu, awaachilie mateka na kuwaamsha wazembe, ili wote waweze kubarikiwa kwa kumbukumbu na sifa Yako.  
Wewe ndiye Mwenye uwezo na Mwenye nguvu.

-`Abdu'l-Bahá
-----------------------

SALA KWA WATOTO NA VIJANA (#11219)

Ee Mungu, niongoze, nilinde, nifanye taa inayowaka na nyota ing’aayo.  Wewe ni Mwenyezi na Mwenye nguvu.

-`Abdu'l-Bahá
-----------------------

